Transcribed

Mti wa Ujuzi - 3. Maarifa (Ujuzi), Mema na Mabaya (Seh. 3)

Mar 17, 2024 · 1h 26m 50s
Mti wa Ujuzi - 3. Maarifa (Ujuzi), Mema na Mabaya (Seh. 3)
Description

Maarifa ya ndani ni kazi ya kiungu ndani ya mwanadamu. Maarifa haya hayahusiani na akili (intellect). Maarifa ama ujuzi hufahamika kwa Kiebrania kama "Daath". Maarifa yanaweza kusababisha uzima ama mauti...

show more
Maarifa ya ndani ni kazi ya kiungu ndani ya mwanadamu. Maarifa haya hayahusiani na akili (intellect). Maarifa ama ujuzi hufahamika kwa Kiebrania kama "Daath". Maarifa yanaweza kusababisha uzima ama mauti kwa mtu, itategemeana na kazi za matendo yake. Katika masomo haya, tunapata kuona ya kwamba Muumba huumba kwa kupitia Maarifa na kwamba Muumba ndani yetu ni yule hufahamika kama Ruach Elohim (ama Ruach El Ha'yam). Idadi ya neno "Ruach Elohim" katika hesabu za herufi hizo ni jumla 300.

Hii 300 ni thamani ya herufi ya Kiebrania Shin ש amapo herufi hii huwa na maana ya moto. Huu ndiyo moto ambao hufanya kazi ndani ya kila mtu. Hii ni sababu pekee ya kwamba tunapotizama neno mwanaume kwa Kiebrania ni neno "ish איש", kadhalika neno mwanamke kwa Kiebrania ni neno "ishah אשה". Tunaposoma kitabu cha Mwanzo (Bereshit) tunajifunza kwamba wawili hawa hawaitwi Adam wala Eva isipokuwa ni baada ya kufukuzwa ndani ya bustani.

Vile vile tunapotizama neno mwanaume yaani ish איש tunagundua kwamba tukiondoa herufi Yod י kinachosalia husomeka "esh אש" ambayo ina maana ya "moto", kadhalika neno mwanamke yaani ishah אשה tukiondoa herufi Hei ה tunasalia na neno "esh אש" ambalo lina maana ya "moto".

Yod י ni herufi kiume enye maana ya uume. Kadhalika Hei ni herufi kike enye maana ya uke. Hizi ndizo tofauti kuu za msingi zinazotofautisha mwanaume na mwanamke yaani kwa maana ya jinsia.

Moto huu ni kazi ya Ruach Elohim ambaye ni baba aliye sirini kwa kila mtu. Moto huu unapotumiwa kwa usahihi yaani kwa mema (tov טוב) huwa ni sababu ya wokovu kwa nafsi lakini unapotumiwa kimakosa yaani kwa mabaya (ra רע) huwa ni sababu ya kuangamia kwa nafsi.

Karibu kujifunza maarifa haya kwa kina.

Ikiwa una maoni ama maswali ama ushauri, tuandikie kwa baruapepe ya:
tanzaniagnosishelpers@gmail.com


Maarifa nuwa na matokeo ya moto
show less
Information
Author Tanzania Gnosis
Organization TanzaniaGnosis
Website -
Tags
-

Looks like you don't have any active episode

Browse Spreaker Catalogue to discover great new content

Current

Podcast Cover

Looks like you don't have any episodes in your queue

Browse Spreaker Catalogue to discover great new content

Next Up

Episode Cover Episode Cover

It's so quiet here...

Time to discover new episodes!

Discover
Your Library
Search