Mti wa Ujuzi - 2. Maarifa (Ujuzi), Adam na Eva ndani yetu
Download and listen anywhere
Download your favorite episodes and enjoy them, wherever you are! Sign up or log in now to access offline listening.
Mti wa Ujuzi - 2. Maarifa (Ujuzi), Adam na Eva ndani yetu
This is an automatically generated transcript. Please note that complete accuracy is not guaranteed.
Description
Tunapozungumzia Adam tunapata tafsiri ya mwanaume, kadhalika Eva, mwanamke. Katika maarifa ya ndani tunapata kufahamu ya kwamba Adam na Eva ni uhusika ambao unakamilisha uhalisia wetu sisi wenyewe. Adam na...
show moreKwa kuzingatia hayo, vile vile ni muhimu sana kufahamu ya kwamba Adam na Eva ndani ya miili yetu huwakilishwa na UBONGO na VIA VYA UZAZI. Adam kama ubongo iwe no ubongo wa mwanaume ama wa mwanamke, na Eva kama via vya uzazi, iwe ni via vya uzazi vya kike ama vya kiume, vyote husimama nafasi ya Eva.
Eva (via vya uzazi) anajaribiwa na kula tunda la mti wa ujuzi wa mema na mabaya lakini pia ili ampatie Adam (ubongo) ili naye ale inampasa kunyosha mkono (kwa kupitia uti wa mgongo ambao una pingili 33). Hizi pingili 33 katika maarifa ya kinumerolojia ndani ya Kabbalah ni sawa na 3+3 ambayo ni 6. Uti wa mgongo katika maarifa ya Kabbalah huwakilishwa na herufi Vav (ו) ya Kiebrania ambayo vilevile ni herufi ya 6 kimpangilio na ina thamani ya namba 6.
Amri ya 6 inasema "usizini" lakini pia uumbaji unafanywa kwa siku 6 bila kusahau ya kwamba mwanadamu anaumbwa siku ya 6. Karibu ujifunze pamoja nasi katika elimu ya ndani ya Gnosis.
Information
Author | Tanzania Gnosis |
Organization | TanzaniaGnosis |
Website | - |
Tags |
-
|
Copyright 2024 - Spreaker Inc. an iHeartMedia Company