Mti wa Ujuzi - 1. Maarifa (Ujuzi), Mlango
Sign up for free
Listen to this episode and many more. Enjoy the best podcasts on Spreaker!
Download and listen anywhere
Download your favorite episodes and enjoy them, wherever you are! Sign up or log in now to access offline listening.
Mti wa Ujuzi - 1. Maarifa (Ujuzi), Mlango
This is an automatically generated transcript. Please note that complete accuracy is not guaranteed.
Description
Mti wa ujuzi ni elimu ya kiroho inayohusiana na nafsi ya mwanadamu. Mwili wa mwanadamu ni chombo kinachobeba nafsi na roho hivyo hatuwi na miili kana kwamba haina cha kufanya...
show moreKumekuwa mkanganyiko wa mafundisho juu ya elimu nzima inayohusiana na bustani ya Eden pamoja na mwanaume na mwanamke yaani Adam na Eva ndani ya bustani. Vizazi vilivyotangulia vilikuwa na uhodari wa kuficha maarifa kwa maana si kitu ambacho kila akipataye hukitumia kwa mtizamo chanya. Ni watu wachache sana waliochaguliwa ambao waliweza kupana nafasi ya kujifunza. Kwa kipindi kirefu sana kilichopita, maarifa haya yalifundishwa kwa wachache lakini nyakati zimefika, maarifa kufundishwa kwa kizazi hiki cha sasa.
Maarifa ama ujuzi ni neno "Da'ath דעת" kwa Kiebrabia. Neno hili "Da'ath דעת" ni muunganiko wa herufi za Kiebrania tatu: Daleth ד, Ayin na Tav ת. Pia, zingatia kwamba maneno ya lugha ya Kiebrania husomwa kuanzia upande wa kuume (kulia) kuelekea kushoto.
Karibu sana darasani.
Information
Author | Tanzania Gnosis |
Organization | TanzaniaGnosis |
Website | - |
Tags |
-
|
Copyright 2024 - Spreaker Inc. an iHeartMedia Company